Alhamisi , 11th Dec , 2014

Kocha wa mchezo wa Basebal kutoka Zanzibar, Athuman Msabaha ameiomba Serikali na wadau wa michezo nchini kujitokeza kuunga mkono mchezo wa Basaeball ili vijana wengi wacheze mchezo huo.

Akizungumza na East Africa Radio, kocha Msabaha amesema vijana wanauelewa mkubwa katika mchezo huo suala linalopelekea kuwa na timu nyingi za watoto wanaoupenda na kuuelewa mchezo huo.

Msabaha amesema iwapo mchezo huo utaungwa mkono, utaweza kuliokoa taifa kwa kufanya vizuri katika mashindano makubwa ya ndani na nje ya nchi.