
Serengeti Boys
Mwenyekiti wa Kamati ya Soka kwa vijana, Ayubu Nyenzi amesema, ziara ya Serengeti Boys bungeni itakuwa ni morali nzuri kwao kwa kutambulika kwa viongozi wa taifa hivyo wataenda nchini Gabon wakijua wana deni kwa taifa kwa ujumla.
Nyenzi amesema, ziara hiyo itafungua njia kwa watanzania wengi zaidi kujitokeza kwa ajili ya kusaidia timu hiyo ambayo ipo katika maandalizi ya kuelekea katika mashindano hayo mwezi Aprili mwaka huu.
Nyenzi amesema, viongozi wa Bunge wameanza na anaamini wadau wengine wa michezo an watanzania kwa ujumla wataungana kwa ajili ya kuipa sapoti timu hiyo.
"Wabunge wetu wameanza na naamini wadau wengine watajitokeza kwa ajili ya kuweza kuipa morali zaidi timu ambayo inaenda kupambana kwa ajili ya nchi," amesema Nyenzi.
Nyenzi amesema, wanawaomba wadau kuwa pamoja "Bega kwa bega na Serengeti Boys mpaka Gabon kwa mwaka 2017" ili kuhakikisha malengo yanafanikiwa kwa timu hiyo kuweza kulikuza jina la Tanzania kimichezo.