Jumatano , 25th Jan , 2017

Serena Williams amezidi kujiwekea mazingira ya kutaka kutwaa taji la 23 la Gland Slam, baada ya kumchapa Johanna Konta na kutinga nusu fainali ya mashindano ya wazi ya Australia.

Serena Williams

 

Williams ameendelea kucheza kwa kujiamini, na kupiga mipira yenye nguvu tangu michuano hiyo ianze, hivyo ameungana na dada yake Venus, kuingia nusu fainali, na kuweka rekodi ya wote wawili kuwa na umri wa juu ya miaka 35, kwa mara ya kwanza, kuingia hatua hiyo

Williams, alishinda kwa seti za 6-2 6-3, dhidi ya Muingereza huyo, huenda akakutana na dada yake kwenye fainali kwa mara ya kwanza tangu 2009