Mara baada ya kuweka saini ya makubaliano na timu yake mpya Samatta amesema alikuwa na shauku kubwa kutaka kujiunga na klabu hiyo.
kiungo Mohamed Samata
"Mbeya City ni timu ya kisasa na yenye watu muhimu katika soka, mara zote nikiwa mkoani Mbeya tunapopishana nao barabarani au kucheza nao uwanjani nilikuwa na shauku kubwa ya kusakata kabumbu nikiwa na jezi ya dhambarau na kuwa sehemu ya klabu hii mashuhuri", amesema Samatta.
Kiungo huyo Mohamed Samata ni Kaka yake mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayechezea timu ya KRC Genk huko nchini Ubelgiji.
Mbali na hilo Mbeya City pia imeweza kunasa saini ya mshambuliaji Victor Hangaya ambaye alikuwa akichezea Tanzania Prison kwa kupewa mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wana Mbeya hao kuanzia sasa.
Mshambuliaji Victor Hangaya
Kaimu Afisa Habari wa Mbeya City, Shah Mjanja amewatakia kila la kheri wachezaji hao wapya waliojiunga na wenzao katika kuelekea mashindano ya ligi kuu yanayotegemewa kuanza Agosti 26 mwaka huu.