Ijumaa , 25th Dec , 2015

Mshambuliaji wa Tanzania anaechezea Klabu ya Congo DR, TP Mazembe Mbwana Samatta yuko mbioni kwenda kucheza soka barani Ulaya katika Klabu kubwa ya nchini Ubelgiji inayojulikana kama KRC Genk.

Mshambuliaji wa Tanzania anaechezea Klabu ya Congo DR, TP Mazembe Mbwana Samatta yuko mbioni kwenda kucheza soka barani Ulaya katika Klabu kubwa ya nchini Ubelgiji inayojulikana kama KRC Genk.

Kwa mujibu wa Jarida la kuaminika la nchini Ufaransa France, L’Equipe, TP Mazembe na Genk wamefikia makubaliano kwa nyota huyo hatari atahamia Genk Mwezi Januari mwakani kwenye dirisha la Uhamisho likifunguliwa.

Inaaminika Samatta atasaini mkataba wa miaka minne na nusu na Genk ambayo inacheza ligi kuu ya Ubelgiji iitwayo Belgian Jupiler League na wao wapo nafasi ya 6 baada ya Kushinda mechi nane, sare nne na kufungwa nane msimu huu.

Msimu huu, Samatta amewika Afrika akiwa na TP Mazembe kwa kufunga bao 8 kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika na kuwapa ubingwa wao wa tano wa Afrika.

Vilevile Samatha ametinga kwenye tatu bora ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka kwa wale wachezao ndani ya Afrika baada ya kufanya vizuri na klabu yake akiifungia mabao saba yakiwemo mawili kwenye fainali ya klabu bingwa na kuibuka kinara kwa ufungaji.