Ijumaa , 4th Sep , 2015

Mshambuliaji nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuiunga mkono Taifa Stars dhidi ya Nigeria katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika AFCON.

Samatta amesema bado Tanzania ina nafasi licha ya ukubwa wa Nigeria na huenda wakadharau wakijua wanapambana na Tanzania lakini watahakikisha wanapambana na kuhakikisha wanafanya vizuri.

Samatta, Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe pamoja na Mrisho Ngassa anayekipiga Free State Stars ya Afrika Kusini wamejiunga na kambi ya Stars ambayo imewasili nchi baada ya kambi ya siku nane nchini Uturuki kujiandaa na mechi hiyo.