Jumamosi , 18th Apr , 2020

Nyota wa klabu ya Aston Villa ya England na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, amesema licha ya kuwa nyumbani wakati huu wa janga la Corona lakini anafanya mazoezi kutokana na maelekezo ya kocha.

Mbwana Samatta

Akiongea na Kipenga ya East Africa Radio, Mbwana Samatta amesema ni kweli inawapa shida lakini ni lazima kama mchezaji aendelea kujiweka sawa.

''Benchi la ufundi linatutumia program mara kwa mara ambazo inabidi tuzifanyie kazi ili kuwa tayari muda wote ligi ikirejea tuweze kucheza'' - Amesema Samatta.

Zaidi Msikilize hapo chini