
(Baadhi ya Nyota watakao shuka dimbani kwenye michezo ya leo kuwania kufuzu kombe la dunia Qatar)
Mchezo wa kwanza utawakutanisha DR Congo dhidi ya Morocco majira ya saa 12 jioni, huku Mali wakiwa wenye ji wa Tunisia mchezo utakao pigwa majira ya saa 2 usiku na Cameroon watakua nyumbani kuchuana dhidi ya Algeria mchezo huu pia utapigwa majira ya saa 2 usiku.
Na michezo mingine miwili itapigwa majira ya saa 4 na nusu usiku ambapo mafarao wa Misri watakapo wakaribisha mabingwa wa Africa Senegal ikiwa sasa ni mara ya pili nyota wa majogoo wa anfield liverpool mohammed salah ana Sadio Mane wanakutana mwaka huu katika michezo muhimu wakiziongoza timu zao za taifa, ambapo mchezo huu ni kumbukizi ya mchezo wa fainali ya michuano ya mataifa ya Africa AFCON ya mwaka huu.
Senegal wanachotaka hapa ni kuendeleza huzuni kwa Misri baada ya kuwachapa kwa mikwaju ya penati kwenye mchezo wa fainali ya Afcon mwezi february lakini Msri nao wanataka kulipa kisasi kwa kuwatupanje ya kombe la dunia na wao kufuzu Fainali hizo kupitia mgongo wa Senegal. mchezo mwingine utawakutanisha timu ya taifa ya Ghana 'The Black stars' dhidi ya timu ngumu ya Nigeria 'The Super Eagles.