Jumanne , 6th Oct , 2020

Mshambuliaji wa Liverpool, Xherdan Shaqiri amekutwa na maambuzi ya virusi vya Corona na anakuwa mchezaji wa tatu wa klabu hiyo kukutwa na maambukizi hayo.

Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Uswisi Xherdan Shaqiri amekutwa na Covid-19

Shaqiri amekutwa na Covid-19 baada ya kufanyiwa vipimo alipokuwa anajiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya Uswisi siku ya Jumatatu Oktoba 5, 2020.

Shirikisho la soka la nchi hiyo SFA leo Jumanne limetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa mchezaji huyo ana maambukizi ya Corona.

"Xherdan Shaqiri amepimwa amekutwa na Covid-19. Kwa kushauriana na mamlaka ya afya, mchezaji huyo amejitenga", ilisema taarifa hiyo.

Mchambuliaji huyo atakosa michezo mitatu ya timu ya Taifa katika kalenda hii ya kimataifa ya FIFA, ambapo Uswisi itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Croatia na michezo miwili ya michuano ya UEFA Nations League dhidi ya Hispania na Ujerumani.

Shaqiri anakuwa mchezaji watatu wa Liverpool kukutwa na Corona, wachezaji wengine ni Thiago Alcantara na Sadio Mane .

Wachezaji wote watatu wanatarajiwa kucheza mechi ya EPL dhidi ya Everton Oktoba 17, kwani kanuni za wachezaji wenye Corona wanapaswa kujitenga kwa muda wa siku 10.