Ijumaa , 25th Mar , 2022

Mlinzi wa kati wa klabu ya Chelsea Antonia Rudiger sasa atalazimika kupunguza kiasi cha pesa anacho kihitaji ili kukamilisa usajili wake kama atahitaji kuihama chelsea mwishoni mwa msimu baada ya timu zinazo muhitaji kupinga kiasi cha mshahara anacho hitaji kulipwa.

(Antonio Rudiger)

Uongozi wa klabu ya Bayern Munchen wanaamini kwamba Rüdiger ana umri mkubwa ukilinganisha na kiasi cha pesa anachohitaji kulipwa kwa mwezi kiasi kisichopungua paund laki mbili (200,000/-) kwa wiki, pamoja na ada ya uhamisho ya paundi elfu 25, hivyo sasa atalazimika kupunguza mshahara huo ili uhamisho wake uweze kufanyika.

Wakat huo huo miamba ya la liga nao klabu ya Real Madrid ambao walionyesha nia ya kumtaka mlinzi huyo wa kati raia wa ujerumani wao wametangaza kusiirisha kabisa usajili wa mlinzi huyo kutokana pesa anayo hitaji kuwa kubwa na hali yao ya kiuchumi hairuhusu kutoa kiasi hicho cha pesa.

Klabu ya chelsea 'The Blues' walitoa ofa ya pauni laki moja na arobaini (140,000/-) kwa wiki, lakini nyota huyo wa zamani wa Roma anadai kuhitaji dau la zaidi ya pauni laki mbili (200,000/-) pamoja paund elfu 25 kama pesa ya uhamisho. lakini majadiliano yalianza tena kabla ya Krismasi mwezi decembe mwaka jana kwa matumaini kwamba huenda hapo baadae makubaliano yanaweza kufanikiwa na mlinzi huyo akasalia stanford bridge.

(Bruno Fernandez)

Upande mwingine klabu ya manchester united imefikia hatua za mwisho katika makubaliano ya kumpa mkataba mpya wa miaka 5 kiungo wake Bruno Fernandez utakaombakisha katika viunga vya Old Trafford kwa muda mrefu zaidi, mkataba huo ukitajwa kuwa na thamani ya paund million 12 kwa mwaka.