
Kaimu katibu mkuu wa RT Ombeni Zavara amesema, mpaka sasa kwa upande wa kambi ya mbio fupi wamepata wanariadha nane ambao wataanza kambi muda mfupi ujao huku wakiendelea kutafuta wanariadha wa mbio ndefu watakaoweka kambi ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Olimpiki.
Zavara amesema, pia wapo wanariadha watanzania wengine ambao wanaendelea na kambi ya Eldoreti nchini Kenya ikiwa ni maandalizi pia ambao nao wanatafuta viwango kwa ajili ya kufuzu kuweza kushiriki mashindano hayo.
Mpaka sasa RT kwa upande wa uwakilishi katika mashindano ya Olimpiki wana mwanariadha mmoja ambaye ndiye aliyefikia viwango ambaye ni Alphonce Felix aliyeshiriki mbio za Dunia China ambaye alikimbikia kwa saa 2 na dakika 16.