Jumanne , 21st Jun , 2016

Ikiwa imefuzu hatua ya mtoano ya michuano ya mataifa ya Ulaya 2016, kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza Roy Hodgson ameanza tambo za kutoogopa yeyote mbele ya safari atakayepangwa naye.

Kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema timu yake haiofii timu yoyote itakayo pangwa nayo kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya Mataifa Ulaya 2016.

Suluhu ya usiku wa jana dhidi ya Slovakia, umeifanya Uingereza kumaliza nafasi ya pili ya kundi B, na kuwa na uwezekano mkubwa wa kukutana na mshindi wa kundi F kati ya mataifa ya Ureno, Hungary, Iceland au Austria.

Maamuzi ya kufanya mabadiliko ya wachezaji 6 kwenye kikosi cha jana yalikosorewa na waandishi wa habari, lakini kocha huyo alijitetea na uamuzi huo.

Uingereza ilipiga mashuti 30 kwenye mechi zote 3 za kundi B huko, Saint-Etienne na hata mchezo huo wa jana wakitawala kiasi kikubwa, lakini bado safu ya ushambuliaji ina uhaba wa mabao hadi sasa.

Ubunifu wa kina Raheem Sterling anayetokea pembeni na katikati uhaba wa ufungaji alioanao Harry Kane ambaye bado kinda kwa michuano ya kimataifa kumeanza kutoa hofu kwa Waingereza.