Timu ya RollBall ya Tanzania [wenye Blue] wakichuana na Kenya katika moja ya michuano ya kimataifa ya mchezo huo.
Timu ya taifa ya Rollball ya Tanzania inataraji kushiriki michuano ya ubingwa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati itakayofanyika kuanzia mwanzoni mwa mwezi June mwaka huu jijini Nairobi nchini Kenya.
Mjumbe wa kamati ya ufundi ya chama cha rollball nchini ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo Feruzi Juma amesema watakauwa na kikao jumamosi hii ili kupanga mikakati yakuwa na ligi ndogo ambayo ndiyo itatoa wachezaji wa timu ya taifa huku pia ajenda kubwa ikiwa ni kujadili jinsi gani ya kupata udhamini ambao ndio kilio chao kikubwa.
Aidha Juma amesema kwa sasa wakati wakijipanga kwaajili ya ligi ndogo ya mashindano ya taifa ya mchezo huo tayari taarifa zimeshakwenda katika vilabu vyote shiriki na tayari vilabu hivyo vimeshaanza mazoezi tayari kwa mashindano hayo ambayo pamoja na kutoa bingwa wa nchini wa mchezo huo lakini lengo lake kuu kubwa ni kuteuwa kikosi bora cha wachezaji wa timu ya taifa watakaokwenda kushiriki michuano hiyo.
Juma amesema kwa sasa wachezaji wote baada ya kupokea taarifa hiyo wanafanya mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha wanamshawishi kocha ama benchi la ufundi kuwateuwa katika timu ya taifa ambapo alisema kushiriki na kufanya vema katika michuano hiyo mikubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutafungua fursa ya Tanzania kushiriki michuano mikubwa zaidi yakimataifa.