Jumanne , 19th Jul , 2016

Baada ya ujio wa Alvaro Morata ndani ya klabu ya Real Madrid, James Rodrigues anataka kuondoka ndani ya klabu hiyo, lakini kocha Zinedine Zidane, amesema hawezi kumwachia mshambuliaji huyo.

Kocha wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amekataa amesema upana wa kikosi alichonacho na mahitaji yake unamfanya ashindwe kung'amua mustakabali wa mshambuliaji James Rodrigues ndani ya klabu hiyo.

Zidane ambaye aliiongoza Madrid kutwaa taji la klabu bingwa barani Ulaya msimu uliopita, ameonekana kushindwa kutoa kauli ya kumruhusu nyota huyo kuondoka lakini amesema hawezi kumhakikishia kuanza kwenye kikosi chake cha kwanza.

Kocha huyo raia wa Ufaransa ameongeza kuwa mawazo aliyonayo juu ya Rodrigues ni sawa na yale anayowawazia nyota wengine waliopo katika kikosi chake.