
Mjumbe wa kamati ya mashindano ya Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA, Nassor Sharrif amesema, ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa timu za wanaume ambapo Jeshi Stars watacheza na Tanzania Prisons wakati IP Sports wataumana na Chui kwenye viwanja hivyo.
Sharrif amesema, michuano hiyo itakamilika wiki ijayo kwa hatua ya fainali ambapo wanaamini bingwa ataweza kuwakilisha vizuri mkoa katika mashindano mbalimbali.