Alhamisi , 12th Mei , 2022

Alama 875 alizozipata nyota wa Denver Nuggets, Nikola Jokic zimemfanya kutangazwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa mchezaji bora wa msimu wa NBA yaani MVP akiwapiku nyota wawili kutoka Philadelphia 76ers Joel Embiid na Giannis Antetokounmpo wa Milwaukee Bucks.

(Mchezaji wa Denver Nuggets Nikola Jokic)

Mserbia huyo mwenye miaka 27,anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya NBA kufunga alama 2000,kuchukua rebounds 1000 na kutoa pasi za usaidizi wa mabao yaani (assist ) mara 500 kwa msimu huku akiweka rekodi ya kuwa na wastani wa kufunga alama 25,kuchukua rebound 13 na kutoa pasi za usaidizi wa mabao mara 6 kwa kila mchezo .

"sijui kitu gani unaweza kumzungumzia Nikola kwa wakati huu,kila siku amekuwa na muendelezo na amekuwa akiwaonesha wale wanaompinga jinsi gani mchezaji mzuri anatakiwa kuwa kwa kuonesha kiwango kizuri kwa kila mchezo anapocheza kila siku”amesema kocha mkuu wa Nuggets Michael Malone.

Kwenye michezo ya NBA Playoff,mabingwa watetezi wa NBA Milwaukee Bucks wameifunga Boston Celtics kwa alama 110 dhdi ya 107 na sasa kuongoza kwa michezo 3-2 kutoka kanda ya Mashariki huku upande wa kanda ya Magharibi,Memphis Grizzlies wamewalaza Golden State Warriors kwa alama 134 dhidi ya alama 95 na  sasa kusalia matokeo kuwa 3-2.