Alhamisi , 8th Jan , 2015

CHAMA cha mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam BD, kimesema kimejipanga kizimiliki changamoto zote zitakazojitokeza katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es salaam RBD, katika mzunguko wa pili unaotarajiwa kuendelea hapo Kesho Uwanja wa ndani wa Taifa

Akizungumza na East Africa Radio, Mkurugenzi Mtendaji wa RBA, Mohamed Tajiri amesema wanaamini kuwa kila jambo huwa na changamoto ambazo kama zisipotatuliwa zinaweza kurudisha nyuma michezo hapa nchini suala ambalo kwa upande wao wamejipanga kwa ajili ya kupingana na changamoto hizi na kuweza kuukuza mchezo huu wa Mpira wa kikapu kwa Mkoa wa Dar es salaam na nchi kwa ujumla.

Tajiri amesema, katika kuhakikisha wanakuza mchezo huo, baada ya kumaliza RBA, wanatarajiwa kuanza kuzunguka katika shule mbalimbali hapa nchini wakiwa na washindi wa Ligi hiyo wakiwa na lengo la kutoa mafunzo kwa shule hizo ili kuweza kupata vipaji vipya na vya kudumu hapa nchini.

Tajiri amesema, wanaamini wanaamini mchezo huu unaweza kukua nchini kwa kutafuta vipaji vipya vitakavyoweza kuendelezwa ambapo watapata timu ambazo zitakuwa na uwezo wa kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.