Jumatano , 15th Jun , 2016

Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Leicester City wataanza kampeni ya kutetea taji lao kwa msimu wa 2016/2017, watakaposafiri hadi Hull City, wakati Jose Mourinho ataanza kibarua na Manchester United watakapo alikwa na Bournemouth.

Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza Leicester City wataanza kampeni ya kutetea taji lao kwa msimu wa 2016/2017, watakaposafiri hadi Hull City, wakati Jose Mourinho ataanza kibarua kama kocha mpya wa Manchester United watakapo alikwa na Bournemouth.

Pep Guardiola akiwa kocha mpya wa Manchester City na kibarua chake cha kwanza kwenye ligi kuu ya soka nchini Uingereza, ataanzia nyumbani dhidi ya Sunderland, huku Antonio Conte naye akianza kibarua na Chelsea nyumbani dhidi ya wagonga nyundo, West Ham United.

Arsenal wataanzia nyumbani dhidi ya Liverpool, kwenye mechi hizo zitakazopigwa mwishoni mwa juma, kati ya Agosti 13 na 15, baada ya kutolewa ratiba hiyo, hii leo.