Jumatatu , 25th Mar , 2024

Aliyekuwa mlinzi wa zamani wa klabu za Simba SC na Yanga SC Mrundi Ramadhani Wasso Ramadhani amefariki dunia leo Machi 25-2024 akipatiwa matibabu hospitalini nchini kwao Burundi.

Ramadhani Wasso alikuwa ni mchezaji pekee wa kigeni aliyekuwepo kwenye kikosi cha Simba SC kilichoivua ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika  Zamalek ya Misri msimu 2003-04 na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa barani Afrika .

Atakumbukwa kwa kisa chake cha msimu 2004-05 kugoma kusaini mkataba mpya ndani ya Simba SC kwamba anaenda Ubelgiji kabla ya kutimkia ndani ya Yanga kwa msimu huo na kusaini kandarasi ya miaka 2 kwa vijana hao wa Jangwani.