Ijumaa , 18th Oct , 2024

Ramadhani Kayoko amepewa jukumu la kusimamia mchezo wa Simba SC dhidi ya Yanga SC siku ya kesho saa 11:00 jioni uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam. Simba SC itakuwa wenyeji wa mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara.

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imemtangaza Ramadhani Kayoko kusimamia sheria kumi na saba kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo mchezo unaozikutanisha timu za Simba SC dhidi ya Yanga SC katika uwanja wa Benjamini Mkapa. Mchezo huo mkubwa nchini Tanzania na Afrika ya Masharaiki utachezwa kesho Jumamosi saa 11:00 jioni. Watakaomsaidia Kayoko ni Mohamed Mkono kutoka Tanga na Kassim Mpanga huku Tatu Malogo atakuWa Muamuzi wa mezani.

Mchezo wa Dabi ya Kariakoo utachezwa kesho siku ya Jumamosi saa 11: 00 jioni uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Bodi ya Ligi Kuu Tanzania bara imemtangaza Refarii Ramadhani Kayoko kusimamia mchezo huo. Wasaidizi wa Kayoko siku ya kesho ni Mohamed Mkono na Kassim Mpanga huku Tatu Malogo akiwa Muamuzi wa mezani.

Mchezo wa Dabi ya Kariakoo utaozikutanisha timu za Simba SC dhidi Yanga  SC ni mchezo mkubwa Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla. Mchezo huo umetajwa kuwa ni moja kati ya michezo mikubwa kwa sasa bara la Afrika huku ikishika nafasi ya tano katika michezo inayofuatiliwa na yenye mvuto zaidi.

Simba SC itakuwa timu Mwenyeji wa mchezo huu  na itaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo mitatu mfululizo ya dabi dhidi ya Wapinzani wao wa siku ya kesho timu ya Yanga. Mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi na Wanachi Wametambiana kuelekea mchezo huo kwa  kusema timu yao ni bora kuliko Wapinzani wao na wanauhakika wa kuondoka na ushindi katika mchezo huo.

Mara ya mwisho timu ya Simba SC kuifunga Yanga ilikua msimu wa 2022-2023 ilipata ushindi wa goli 2 waliofunga siku hiyo ni    Enock Inonga Baka na Kibu Dennis. 

Ligi Kuu Tanzania bara inarejea leo Oktoba 18, 2024 baada ya kupisha michezo ya Timu ya Taifa, michezo mitatu imatarajiwa kuchezwa viwanja tofauti. Coastal Union dhidi ya Dodoma jiji utachezwa Sheikh Amri Abeid, JKT Tanzania dhidi ya Tabora utachezwa uwanja Meja Jenerali Isamuhyo na Tanzania Prison dhidi ya Azam utachezwa uwanja wa Sokoine Mbeya.

ligi itaendelea kesho kwa michezo kuchezwa viwanja tofauti Pamba FC dhidi ya Kagera Sugar utachezwa uwanja wa CCM Kirumba, Singida Black Stars dhidi ya Namungo utachezwa uwanja wa Liti na Simba SC dhidi ya Yanga utachezwa uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.

Simba SC imeshacheza michezo mitano ya ligi msimu huu wa 2024-2025 inashika nafasi ya pili ikiwa imekusanya alama 13, Wapinzani wao siku ya kesho Yanga SC imecheza michezo minne ikishika nasafi ya nne ikiwa imekusanya alama 12. Mchezo wa kesho Jumamosi unavuta hisia za Wadau wa Soka nchini Tanzania kutokana na usajili ambao Wekundu wa Msimbazi wameufanya msimu huu ambao unawapa matumaini  Mashabiki wa timu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Msimbazi Karikaoo ya kushinda mchezo wa Dabi siku ya kesho.