Jumanne , 26th Sep , 2023

Rais wa klabu ya Tigres FC inayoshiriki Ligi daraja la pili nchini Colombia, Egdar Paez amepigwa risasi na kufariki baada ya timu yake kupoteza kwa goli 3-2 wakiwa nyumbani dhidi ya Atletico FC na kuifanya Tigres kushuka hadi nafasi ya 15 katika msimamo katika timu 16 za ligi hiyo.

Paez (63) alivamiwa na vijana wawili waliokuwa kwenye pikipiki akiwa kwenye gari lake na binti yake wakirudi nyumbani nje kidogo ya uwanja. Taarifa za jeshi la Polisi nchini Colombia zinasema mtoto wake alitoka akiwa mzima na mamlaka zinaendelea na zoezi la upelelezi kwa waliohusika.