Aliyekuwa rais wa FIFA Sepp Blatter
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema kuwa atajiuzulu kama Rais wa shirikisho hilo kufuatia kashfa ya ufisadi.
Akitangaza kujiuzulu, kwake Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameitisha kikao cha dharura mara moja ili kumchagua Rais mpya.
Blatter alichaguliwa tena wiki iliopita licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi lakini alisema kuwa mamlaka yake hayaungwi mkono na kila mtu.
Shirikisho la FIFA lilikumbwa na mgogoro wa kukamatwa kwa maafisa wake kutokana na mashtaka ya ufisadi ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliofunguliwa na Marekani.
Uchunguzi mwingine unafanywa na serikali ya Switzerland kuhusu namna ambavyo michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 na 2022 ilitolewa pia unavyoendelea. ''Nimehusika sana na FIFA na maslahi yake. kilicho muhimu kwangu ni taasisi ya FIFA na Soka duniani''
Hata hivyo Marekani imeanza kumfanyia uchunguzi kutokana na tuhuma zinazomkabili kwa sasa.