Jumatatu , 18th Mar , 2024

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mussa Azan Zungu amesema katika kuelekea miaka mitatu ya Mheshimiwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassani katika sekta ya michezo ni kutoa kwake hamasa kumevunja rekodi ya kuingiza timu mbili za Yanga SC na Simba SC.A

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 18,2024 Naibu Spika Mheshimiwa Zungu amesema kuwa hamasa zimechangia kiasi kikubwa kufanya vyema kwenye michezo na hii inaonyesha kuwa Rais ana upendo anajitoa kwa wanamichezo katika kuhakikisha hawakumbani na changamoto yoyote wanapokwenda kushiriki michuano mbalimbali.

“Hii ni mara kwanza kwa nchini yetu kufanya vyema hivyo hii hamasa ya Rais kununua mabao imechangia kwa kiasi kikubwa kuzifanya timu zetu kujituma na kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya Taifa “amesema Zungu .

Kwa upande mwingine Naibu Spika huyo amesema Bunge la Tanzania limeenda mbio za marathan zenye lengo la kukusanya zaidi ya bilioni nne kwaajili ya kujenga shule vipaji maaalmu ya bunge ya wavulana ya kidato cha tano na cha Sita zitazofanyika Aprili 13 mwaka huu.

Katika mbio hizo za Bunge Marathan kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa washindi na washiriki kwa kuwapa fedha taslimu pamoja na medali za dhahabu ,Fedha na shaba nazitatolewa kwa mshindi wa kwanza,wa pili,na mshinidi wa tatu.