Jumatano , 17th Feb , 2016

Klabu ya PSG ya Ufaransa imepata ushindi dhidi ya Chelsea mechi ya mkondo wa kwanza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya,baada ya kuitandika mabao 2-1 jijini Paris usiku wa jana.

Paris St-Germain walichukua uongozi kupitia mshambuliaji matata wa Sweden Zlatan Ibrahimovic dakika ya 39,kabla ya Chelsea kusawazisha katika dakika ya 45 kupitia kwa Mikel Obi.

Bao hilo la Mikel ndilo lake la sita kufungia Chelsea katika karibu miaka 10 aliyokaa katika klabu hiyo ya Uingereza

Edison Cavan akaitumia dakika ya 78 kuwaumiza Chelsea,bao la pili na la ushindi,matokeo ambayo hata hivyo kocha wa PSG Laurent Blanc hakufurahia,kwa sababu bao la Chelsea litawapa nguvu kwenye mchezo ujao.

Benfica nao wakilaza Zenit St-Petersburg bao 1-0 ugenini bao lililofungwa na Jonas muda wa ziada kutokana na mkwaju wa adhabu uliopigwa na Nicolas Gaitan.

Hatua hiyo ya 16 bora inatarajiwa kuendelea tena usiku wa leo kwa michezo miwili kupigwa.

Real Madrid wamesafiri hadi kule Roma nchini Italia kuwavaa AS Roma,mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Stadio Olimpico,wakati mchezo mwingine unawakutanisha KAA Genk ya Ubelgiji ikiwaalika VFL Wolfburg kutoka Ujerumani.