
Kocha msaidizi, Juma Mwambusi
Mwambusi amesema hayo muda mchache baada ya kikosi chake kuwasili katika viunga vya uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wao wa kesho wa kusaka alama tatu za ushindi.
"Kagera Sugar ni timu yenye uwezo mkubwa na tunatambua hilo, kikubwa ni kwamba mchezo wa kesho siyo mchezo rahisi na tumejipanga vyema kupambana na Kagera Sugar....Haijalishi matokeo ya mchezo wa kwanza ambao tuliwafunga goli 6 bali tunaangalia kupata pointi 3 ambazo ni muhimu sana kwetu kwenye kutetea ubingwa wetu wa Ligi kuu Tanzania Bara".Alisema Mwambusi
Katika hatua nyingine, msimamo wa ligi kuu mpaka sasa Simba SC ndiyo anaongoza Ligi akiwa na alama 62, ikifuatiwa na Yanga ikishika nafasi ya pili kwa pointi 59, Azam FC wakiwa nafasi ya tatu kwa pointi 49 huku Kagera Sugar wakiwa nafasi ya nne kwa alama 47.