Alhamisi , 25th Nov , 2021

Mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amemshauri kocha wa PSG Mauricio Pochettino kujiunga na Manchester United kuchukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer aliyetimuliwa kazi baada ya kuwa na matokeo mabaya ndani ya kikosi hicho.

Kocha wa PSG Mauricio Pochettino

Ushauri wa Carragher ameutoa baada ya PSG kukubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa Manchester City kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya huku akisemaPochettino anapaswa kutoka na kwenda klabu nyingine,kama akipata hiyo nafasi ni bora aende tu maana ningekuwa mimi ningekwenda hata kesho”.

Carragher anaamini kitendo cha Pochettino kama atakubali kujiunga na United kutamsaidia kukua kwenye nyanja yake ya ukufunzi wa soka huku gwiji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry akimuunga mkono Jamie Carragher kuhusu kuondoka kwa kocha huyo na kwenda kutafuta changamoto mpya nje ya PSG.

Kwa mfumo uliopo Pochettino hawezi kuwa Pochettino kwenye timu hii,Unawezaje kuwaweka benchi wachezaji (Messi, Mbappe au Neymar)? Analazimika kumtumia Angel Di Maria katika sehemu ya kiungo jambo ambalo halimsaidii na kuifanya timu kuwa wazi zaidi”.amesema Henry

Kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne,Pochettino alisema ana furaha ndani ya PSG kwani ni fahari kwake kuwa kocha na pia aliitumikia kama mchezaji na bado ana furaha kuwa sehemu ya familia ya PSG