
Rais wa shirikisho la soka la bara la Ulaya ambaye amesimamishwa Michel Platini amesema hatawania urais wa Fifa katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao.
Platini, pamoja na rais wa Fifa Sepp Blatter wamefungiwa kutojihusisha na shughuli za soka kwa miaka nane na shirikisho hilo linalosimamia soka duniani kwa makosa ya ulaji rushwa inayohusiana na malipo ya pauni milioni1.3m kwa Platini mwaka 2011.
Katika taarifa yake Platini amesema amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwa rais wa Fifa kwa kuwa hakupewa muda wa kujiandaa kupambana na wengine
Hata hivyo viongozi hao wawili Wamekata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka nane na sio kutaka kuwahi uchaguzi huo.