Guardiola ameweka wazi kuwa watamkosa kiungo huyo raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 28 kwa kipindi kirefu, lakini bado hawajajua ni muda gani atakuwa nje ya uwanja. kwa sasa Rodri ameenda nchini Hispania kwa Uchunguzi zaidi na baada ya hapo watajua atafanyiwa upasuaji wa aina gani na atakuwa nje kwa muda gani
Rodri ambaye jina lake kamili ni Rodrigo Hernández amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Man City kwa mujibu wa takwimu. Kwenye michezo 48 ambayo ameanza kwenye kikosi cha City hawajafungwa mchezo hata mmoja na msimu uliopita Man city ilipoteza mchezo 1 tu kati ya michezo 50 ambayo Rodri alikuwepo. Na City Ilifungwa michezo 4 kati ya 5 waliyocheza bila ya uwepo wa Rodri.