
Barcelona wakishangilia baada ya Messi kupiga bao la pili
Barca walikuwa wa kwanza kufunga katika Dakika ya 4 kupitia Messi, aliyemegewa pasi nzuri na Luis Suarez, lakini Leganes wakasawazisha dakika ya 71 kwa bao la unai Lopez.
Baadaye Barca wakapata ushindi baada ya Penati iliyotolewa baada ya Neymar alipoangushwa ndani ya boksi, na Messi kuipiga kiufundi kwa guu lake la kushoto, kunako dakika ya 90.
Wiki iliyopita haikuwa njema kwa Barca kwani Jumanne iliyopita walicharazwa 4-0 na Paris Saint-Germain katika Mechi ya kwanza ya raundi ya mtoano ya timu 16 za UEFA Champios League, iliyochezwa huko Paris, France.
Kwenye Mechi hiyo ya jana baadhi ya mashabiki wa Barca waliamua kuizomea timu yao katika dimba la Nou camp
Ushindi huu wa Barca dhidi ya Leganes umewaweka nafasi ya pili Pointi 1 nyuma ya Real Madrid wenye mechi 2 mkononi na hivyo kuendeleza ushindani katika mbio za ubingwa wa La Liga msimu huu.