Jumatatu , 8th Aug , 2016

Kiungo wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Juventus ya Italia, Paul Pogba ameruhusiwa kufanya vipimo vya afya Old Trafford ikiwa ni moja ya ishara kuwa huenda Manchester United imeafikiana na wakala wake kumnunua mchezaji huyo.

Mshambuliaji wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Juventus ya Italia, Paul Pogba.

Pogba mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akizungumziwa sana kuhusu kuhamia Old Trafford kwa bei ya kuvunja rekodi ya dunia ya ununuzi wa wachezaji ya pauni milioni 100.

Aidha, Pogba aliichezea Manchester United kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Italia, Juventus na alicheza katika mechi 3 pekee akiwa klabuni hapo.

Jana baada ya mechi kati ya Man United na Leicester City katika uwanja wa Wembley kocha wa Manchester United Jose Mourinho alisema kuwa Man united ni klabu sahihi na ligi kuu ya England itakuwa ni hatua bora kwa ajili Pogba.

"Tuna kila kitu cha kumpa, na sisi tunajua sababu kwa nini anataka kuja kwetu," alisema Mourinho.

"Yeye anakuja kwa sababu anaijua klabu, anaujua mji vizuri pia anawajua wachezaji wengi katika klabu hii hivyo anataka kuwa sehemu muhimu Man United"- Mourinho.

Juventus wataanza msimu wao Serie A wiki moja baadaye tarehe 20 Agost.