Jumanne , 27th Dec , 2016

Mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Uganda, Denis Masinde Onyango amewekwa kwenye 10 bora ya walinda mlango wa mwaka 2016.

Mlinda mlango wa Uganda Cranes Denis Onyango

 

Onyango anayedakia kwenye klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, anakamata nafasi ya 10, akiwa na pointi 5, akichaguliwa na shirikisho la kimataifa la historia na takwimu ya mpira wa miguu (IFFHS).

Onyango alitwaa ubingwa wa Afrika na ligi kuu ya soka Afrika Kusini akiwa na Mamelod, huku pia akiwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anayesakata kabumbu, ndani ya Afrika.

Onyango amewapita makipa bora kabisa Duniani, Petr Cech wa Arsenal na Marc Andre Ter Stegen wa Barcelona wanaoshika nafasi ya 11 na 13.

Nafasi ya kwanza ya mlinda mlango bora duniani kwa sasa inaendelea kushikiliwa na mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich Manuel Neuer.