Jumatano , 13th Jun , 2018

Kuelekea msimu mpya wa mashindano ya Sprite Bball Kings yanayoandaliwa na East Africa Television Limited kwa kushirikiana na Kampuni ya Cocacola kupitia kinywaji cha Sprite, watakao kuwa bora huenda wakapata safari ya Marekani.

Akiongea kuhusu zawadi za wachezaji bora akiwemo Most Valuable Player na wengine watakaofanya vizuri, Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa Kikapu nchini (TBF), amesema wao kama shirikisho watajipanga kuona namna ya kuwazawadia.

''Kama shirikisho nasi tutaona namna nzuri ya kutoa zawadi kwa watakaofanya vizuri. Ni vyema tukawasogeza hata Marekani wakaenda kuona wenzao wanafanyaje, hilo lipo ndani ya uwezo wetu kama TBF kwa kushirikiana na serikali tunaamini litafanikiwa'', alisema.

Ikumbukwe mwaka jana mchezaji wa timu ya Mchenga BBall Stars Rwahabura Munyagi aliibuka 'MVP' huku mabingwa wakiwa ni Mchenga BBall Stars na mshindi wa pili akiwa ni TMT.

Usaili wa timu zitakazoshiriki Mashindano ya Sprite Bball Kings 2018, utakuwa ni mmoja pekee na utafanyika siku ya Jumamosi Juni 16, wiki hii Katika viwanja vya Mlimani city Mall, Dar es salaam, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Njoo na majina ya timu yako uweze kuandikisha. Mashindano ya Sprite Bball Kings yameletwa kwenu kwa udhamini wa sprite. Sprite, Kiu yako kwanza.