Ijumaa , 9th Feb , 2018

Kuelekea mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika kesho klabu ya Yanga imepata nguvu mpya baada ya nyota wake saba waliokuwa majeruhi kurejea mazoezini leo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya  St. Louis. 

Akitoa ripoti leo daktari wa timu hiyo Dr. Edward Bavu amesema wachezaji hao ambao ni miongoni mwa wachezaji 11 waliokuwa majeruhi wamepona na wapo tayari kuendelea na majukumu yao uwanjani.

''Wachezaji saba kati ya 11 wamepona na leo asubuhi wamefanya mazoezi na wenzao hivyo tunasubiri mwalimu kuona kama wapo 'fit' kucheza mana pia ni maamuzi ya mwalimu kutokana na namna alivyofanya mazoezi na kikosi'', amesema.

Wachezaji ambao wamerejea kukipa nguvu kikosi cha Yanga ni Youthe Rostand, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vicent, Pato Ngonyani, Thaban Kamusoko na Ibrahim Ajib.

Ambao bado ni majeruhi amewataja kuwa ni Donald Ngoma, Abdalah Shaibu, Yohana Mkomola, Amissi Tambwe. Yanga kesho inacheza mchezo wake wa kwanza ligi ya Mabingwa dhidi ya St. Louis  ya Shelisheli.