Ijumaa , 21st Mei , 2021

Klabu ya Wolves imetangaza kuondoka kwa kocha wa timu hiyo Nuno Espirito Santo mwishoni mwa msimu huu, na wadau wengi wameanza kumuhusisha kwenda kua kocha wa Tottenham Hospurs msimu ujao.

Kocha Nuno Esoirito Santo

Nuno Espirito Santo ataondoka Wolves baada ya mchezo wa mwisho wa Jumapili wa msimu dhidi ya Manchester United. Bosi huyo wa Ureno anaondoka kwa kukubaliana baada ya miaka minne ya uongozi ambao ameongoza klabu hiyo kupanda ligi kuu ya England na kumaliza ligi katika nafasi ya saba, kabla ya kua na msimu usiokuwa na matokeo ya kuridhisha kwa upande wao.

Nuno sasa ameanza kutajwa kama kipaumbele katika nafasi ya kuchukua mikoba ya jose mourinho katika klabu ya Tottenham msimu ujao.