Wachezaji wa Njombe Mji wakielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo katika mechi dhidi ya Makambako United katika uwanja wa Aamani Makambako
Akizungumza na East Africa Radio mwenyekiti wa klabu hiyo Erasto Mpete amesema lengo lao ni kuhakikisha timu yao inaweka rekodi ya kushiriki kwa mara ya kwanza ligi hiyo na kukwea hadi ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa msimu ujao.
Mpete amesesetiza wakazi wa Njombe wanakiu ya kushuhudia mechi za ligi kuu ya soka Tanzania bara mkoani mwao hivyo wao kama Viongozi hawana budi kushirikiana na wadau pamoja wachezaji katika kuweka mkakati wa ushindi katika kila mechi.
Mji Njombe imeendelea kung'ang'ania nafasi yao ya pili baada ya hapo jana kuichapa Kurugenzi ya Mkoani Iringa bao 2-1 na kufikikisha pointi 16 huku wakiifukuza Ruvu Shooting iliyoinyuka Mlale Jkt jana bao 3-0 na kufikisha pointi 19.