Akiongea katika mkutano na wanahabari leo Niyonzima amesema amejiandaa vyema yeye pamoja na wachezaji wenzake katika kupambana na wapinzani wao huku shabaha yao ikiwa ni kufuta historia ya kufungwa na wanalambalamba kutoka vingunguti.
"Namshukuru Allah binafsi nipo vyema kwa ajili ya mchezo wa kesho, mwalimu akinipa nafasi hakika nitatimiza majukumu yangu vyema pamoja na wenzangu ili kuhakikisha timu yetu inashinda". Alisema Niyonzima

Kikosi cha Yanga
Aidha Nahodha huyo amejigamba kwa kusema walimu wao wamewaandaa vyema katika kutetea ubingwa wao katika mchuano huo pamoja na mashindano yao mengine huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa ushirikiano ili kuwatia nguvu kwa dakika zote 90 za mchezo.
Mchezo huo utarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, majira ya saa kumi





