Nico Rosberg akiruka juu kwa furaha mbele ya mshindi wa pili Sebastian Vettel (kushoto) na Sergio Perez
Nico Rosberg ametwaa taji la Europian Grand Prix, huku Dereva mwenza wa timu ya Mercedes, Lewis Hamilton akimaliza nafasi nafasi ya 5.
Rosberg aliongoza toka hatua ya mwanzo na kushinda taji la tano la formula 1 kwa msimu huu huko mji wa Baku, Azerbaijan.
Kushindwa kwa Hamilton, kunamfanya apoteze pointi 24 kwa Rosberg.
"Wikiendi iliisha vizuri".' Ilikuwa ya kushangaza, hivyo ninafuraha sana. Naburudika na ushindi huu, sherehe kubwa". Alisema Roseberg.

