Mshambuliaji wa Yanga, Said Ntibazonkiza.
Akizungumza na East Africa Radio, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema baadhi ya wachezaji hao wa kigeni wanamalizia mechi za mataifa yao ambayo yanawania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika leo na kwa mujibu wa tiketi zao wataungana na wenzao siku mbili zijazo.
''Wachezaji waliokuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania''Taifa Stars'' walishawasili tangu siku ya Jumatatu, wakati Saido Ntibazonkiza(Burundi), Tomombe Mukoko(Dr Congo) na Haruna Niyonzima (Rwanda) wataanza kuwasili siku ya Alhamis.
Yote kwa yote timu yetu inaendela vyema na mazoezi chini ya kocha Juma Mwambusi, tupo kileleni lakini pia bado tunaendelea na mchakato wa kumpata kocha mpya pindi ambapo tutakamilisha tutawatangazia.'' alisema Bumbuli.