Jumatatu , 16th Dec , 2024

Msimu wa sikukuu ndiyo huu, shangwe na furaha zitatawala kwa walio wengi kwenye msimu huu, wapo wa kwenda kutalii, matembezi ya hapa na pale, kukaa ndani na aina nyinginezo za kuupa mwili pole kwa shughuli za mwaka mzima.

 

Sasa wakati unaondoa aibu kwenye kula jasho lako, kuna kitu kimoja inabidi tukumbushane ili tukifika kwenye hayo maeneo ambayo ni mageni kwetu tusionekane sisi ni wakuja.

Kabla ya hatujakumbushana ni kuulize kitu, umekwisha wahi kwenda kwenye eneo la kupata chakula na baada ya kufika tu, unakutana na orodha ya vyakula pamoja na bei lakini hujui chakula husika kinafananaje, kama ulikwisha wahi kutana na hali ya namna hiyo basi leo ndiyo mwisho kwani wanasema ushamba ni wakati wa kwenda tu, ukirudi njia unaijua.

Nataka nikupe njia ambayo itakusaidia kuepuka fedhea ndogondogo pale ambapo utakuwa kwenye mgahawa wa kigeni na hujui utatokaje kwenye hali hiyo.

Kuna hii wavuti ambayo inafahamika kama PICMENU.CO sasa utakachokifanya baada ya kuingia kwenye wavuti hii ni wewe kuchukua orodha ya vyakula ambayo umekutana nayo hapo mgahawani, utapiga picha na kuweka kwenye wavuti hii baada ya hapo wavuti itakusaidia kuleta michoro halisia ambayo inaonesha namna ambavyo chakula husika kinaonnekana na viungo vilivyo tumika kwenye kupika chakula hicho.

Kutokea hapo ni yetu matumaini hutoa agiza tena chakula ambacho usingependa kula baada ya kufika mezani, kwani PICMENU.COM imefanya kazi yake.