Jumatano , 14th Mei , 2014

Mashindano ya masumbwi ya ridhaa ya 'Meya Cup' yanatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 4 mwaka huu jijini DSM.

Mashindano ya masumbwi ya ridhaa ya 'Meya Cup' kuanza baadaye mwaka huu.

Chama cha masumbwi ya ridhaa mkoa wa Da es Salaam DABA, kimeandaa mashindano ya kombe la Meya yatakayoanza tarehe 4 mpaka tarehe Mwezi Juni mwaka huu jijini DSM.

Afisa habari wa DABA Bi. Mwamvita Mtandae Jacob amesema baada ya hali ya sintofahamu kukikumba chama hicho kwa muda mrefu, sasa mambo yamekaa sawa na kinachofuatia ni kuhakikisha mchezo huo unapiga hatua kwa kuwa na mashindano mengi iwezekanavyo wakianza na haya ya kombe la Meya.

Aidha Bi Mwamvita amesema licha ya kwamba wao ni chama cha mkoa na mashindano hayo ni ya Meya wa DSM, lakini wanakaribisha mikoa yote yenye uwezo wa kushiriki na mpaka sasa mikoa minne imekwishathibitisha.

Mikoa hiyo ni Morogoro, Arusha, DSM kama wenyeji na Tanga.