Ijumaa , 13th Nov , 2015

Timu ya taifa ya mchezo wa ngumi imeomba watanzania kujitokeza kwa ajili ya kusaidia vifaa mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu michezo ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika hapo mwakani nchini Brazil.

Kocha wa timu ya taifa ya ngumi Said Omary Gogopoa amesema, timu hiyo inaendelea na mazoezi lakini tatizo kubwa ni ukosefu wa vifaa ambavyo ni muhimu kwa timu hiyo ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano.

Gogopoa amesema, wachezaji wanajituma na wanahakikisha watafanya vizuri katika mashindano hayo na kuweza kushiriki Olimpiki na hata kuweza kurudi na medali.