Jumatatu , 3rd Aug , 2015

Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini BFT limesema, wanaamini timu ya Taifa ya Ngumi itaweza kufanya vizuri katika mashindano ya All African Games yanayotarajiwa kufanyika Septemba nne mwaka huu nchini Congo Brazzaville.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema, Serikali na watu binafsi wanahitajika ili kuweza kuisaidi timu hiyo ambayo imeshariki mashindano ya majaribio ya Afrika Mashariki na kati mwishoni mwa wiki hii n akuweza kushika nafasi ya pili ambayo inaonyesha matumaini kwa timu hiyo kufanya vizuri hapo baadaye.

Mashaga amesema, licha ya changamoto zilizopo katika timu hiyo lakini iliweza kupigana kwa ajili ya kuitetea nchi na kuweza kurudi na ushindi huo lakini bado ipo kambini na mashindano ya Al African Games hayapo mbali hivyo kama itapata msaada wa mapema itaweza kufanya maandalizi ya mapema na kuweza kuitangaza nchi katika ramani ya michezo.