
Alvaro Gonzalez na Neymar Jr wakizozana katika mchezo wa PSG na Marseille
''Baada ya kupitia jalada lao kwa umakini wa hali ya juu,na tumewasikiliza wachezaji wenyewe na wawakilishi wa timu zao,tumejiridhisha hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuwatia hatia'' ilisema taarifa ya kamati hiyo
Katika mchezo wa ligi ya Ufaransa baina ya PSG na Marseille ziliibuka vurugu kubwa sana hali iliyosababisha kutolewa kwa kadi 5 nyekundu, kadi14 za njano na kufanya kuwe na jumla ya kadi 19 katika mchezo moja, huku Neymar akionekana ni chanzo kikubwa wa vurugu hizo
Awali zilitoka adhabu kwa wachezaji 5 waliojihusisha moja kwa moja na vurugu hizo, Layvin Kurzawa amefungiwa mechi 6,Leandro Peredes 3 na Neymar 3 kwa upande wa PSG huku Jordan Amavi na Dario Benedetto wa Marseille wamefungiwa mechi 3