Katika taarifa yake, kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa katika mchezo huo Taifa Queens, Edson Chitanda amesema, wamepewa taarifa ya kubadilishwa sehemu ya mashindano hivyo wanatarajia kuondoka nchini hapo kesho.
Chitanda amesema, timu ipo kambini ambapo inatarajia kuondoka na wachezaji 15 wakiambatana na viongozi wakiwa tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

