Venus Williams (Kushoto) na Serena Williams wakiwa na baba yao, Richard Williams
Venus aliye katika nafasi ya tatu kwenye viwango vya ubora duniani ametinga fainali ya grand slam kwa mara ya kwanza tangu 2009 kwa kumnyuka Coco Vandeweghe kwa aseti 6-7, 6-2 na 6-3 huku Serena anayewania taji la grand slam kwa mara ya 23 amemshinda mcroatia Lucic-Baroni kwa seti 6-2 6-1 asubuhi ya leo.
Hii ni mara ya kwanza kwa ndugu hao kukutana katika fainali ya mashindano ya grand slam katika kipindi cha miaka 8 ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2009 katika mashindano ya Wimbledon na Serena alipata ushindi.
Hii ni mara ya tisa kwa ndugu hawa kukutana katika fainali za grand slam huku takwimu zikionesha kuwa katika michezo 26 ambazo ndugu hao wamekutana, Serena ameshinda michezo 16 na Venus akishinda michezo 11.
Endapo Venus atashinda katika mchezo huo wa Jumamosi atakuwa ndiye mwanadada mwenye umri mkubwa zaidi kushinda taji la grand slma katika open era, wakati Serena akishinda ataweka rekodi ya mwanamke mwenye mataji mengi zaidi ya grand kwa kufikisha grand slam 23.
Mchezo huu utapigwa siku ya Jumamosi, Februari 28 na baadhi ya wadau na wataalamu wa mchezo huo wametabiri ugumu wa mchezo wa fainali hiyo
Hassan Khasim ni mmoja wa makocha wa mchezo wa tenisi na shabiki mkubwa wa wanadada hao amezunguzia fainali hiyo....