Jumamosi , 10th Jul , 2021

Ligi kuu ya kikaou nchini Marekani 'NBA' ni miongoni mwa ligi kubwa Duniani zilizofanikiwa kuendelea na shughuli za michezo kwa kutumia taratibu maalum zilizopelekea ligi hiyo kukosa mgonjwa hata mmoja wa COVID-19 kwa mujibu wa vipimo vya tarehe 30 Juni mwaja huu.

Wachezaji wa timu ya New York Knicks wakiwa wamevaa barako kama tahadhari ya kujikinga na uwezekano kuambukiza na kuambukizwa COVID-19.

Taarifa za vipimo hivyo vimewekwa wazi usiku wa kuamkia leo baada ya jopo la wataalam wa kupima COVID-19 kuwapima wachezaji 106 toke Juni 30, 2021 wanaoshirikishi NBA na kutomkuta mchezaji hata mmoja mwenye maambukuizi ya ugonjwa huo hatari Diniani tokea uibukie China takriban miaka miwili iliyopita.

Majibu ya vipimo hivyo vinaashiria kuwa wasimamizi wa Ligi ya kikapu nchini Marekani wamefanyakazi kubwa ya kusimamia timu zote shiriki kuishi kwa kuzingatia taratibu za kitabibu za kujikinga dhidi ya Covid-19 kwa kupunguza idadi ya mshabiki ili kukwepa msongamano pamoja na wachezaji kuvaa barakoa.

Mbali na kusitisha na baadae kuruhusu mashabiki wachache, Wasimamizi wa NBA pia walikubali kupima afya wachezaji hao mara kwa mara ili kuabini endapo kuna wagonjwa wa ugonjwa huo au laa jambo ambalo lilisidia kuwafanyai wachezaji waishi kwa umakini mkubwa.

Ligi ya kikapu nchini Marekani inatazamiwa kuendelea saa 9:00 usiku wa kuamkia Julai 12, 2021 kwa mchezo wa tatu wa fainali ya ligi hiyo ambapo, timu ya Phoenix Suns wanaongoza series 2-0 dhidi ya Milwaukee Bucks baada ya kuwafunga 118-105 mchezo wa kwanza, 118-108 kwenye mchezo wapili.