Haruna Niyonzima akiwa pamoja na Afisa habari wa Simba, Haji Manara.
Niyonzima ameeleza hayo muda mfupi ulipomalizika mtanange wao wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports FC ya Rwanda.
"Siyo rahisi kutoka Yanga kwenda Simba au kutoka Simba kwenda Yanga lakini yote ni maisha. Naamini kuna wanayanga pamoja na mashabiki wangu wameumia kuniona mimi nacheza Simba lakini niseme kwamba yote ni maisha kwa sababu mimi ni mchezaji wa mpira siwezi kujua nitaishia wapi, kikubwa ni kuifanya kazi yangu", amesema Niyonzima.
Pamoja na hayo, Niyonzima ameendelea kwa kusema "Niishukuru timu ya Yanga unajua ni timu ambayo mpaka sasa hivi nimecheza misimu mingi sana kuliko timu zote duniani 'so' ni kitu cha kuwashukuru nimeishi nao vizuri. Najua katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga haitokuwa mechi rahisi ila natamani japo niwafunge goli ili niwaage kwa heshima".
Kwa upande mwingine, Niyonzima amesema yeye binafsi hakuwa na ndoto za kucheza soka nchini Tanzania ila mipango ya Mungu ndiyo imemfanya awe hapo