
Wachezaji wa Yanga pamoja na benchi la ufundi
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Kipenga cha East Africa Radio, Mwenyekiti wa TPLB Steven Mguto amesema ameshangazwa na kauli zilizotolewa na kocha wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa juu ya upangwaji wa ratiba ambao anaamini uliathiri pia ubora wa timu yake katika mchezo wa juzi waliotoka sare ya bao 1-1 na KMC.
Wakati huohuo nahodha wa Azam Fc, Aggrey Morris alionekana kuitupia lawama bodi ya ligi kwa kubadilishiwa muda wa mchezo wao kati ya JKT Tanzania, ambao ulipigwa saa 10:00 jioni, tofauti na taarifa ya awali ambapo ulipangwa kuchezwa saa 1:00 usiku.
Wakati lawama hizo zikielekezwa kwa bodi huku ikidaiwa kuwa na lengo la kudhoofisha matokeo ya timu hizo, Mwenyekiti wa bodi ya ligi Steven Mguto amesema upo utaratibu wa kutoa malalamiko kikanuni na sio kuongeza kwenye vyombo vya habari .
Kwa maana hiyo hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika ili kuhimiza nidhamu na kufuatwa kwa kanuni zilizowekwa.