Mwamuzi Martine Saanya (Kulia) katika mchezo uliopita, uliozua vurugu na kusababisha mwamuzi huyo kufungiwa
Afisa Habari wa shirikisho hilo, Alfred Lucas amesema wameamua kuficha jina la mwamuzi huyo ili kupunguza uwezekano wa hujuma au hisia za mwamuzi kununuliwa au kusumbuliwa na ama timu mojawapo au timu zote mbili.
Lucas amesema TFF imeamua kujiwekea utaratibu huo ili kuepusha uwezekano wa kutokea kwa vurugu kama zilizotokea katika mchezo uliopita, na sasa timu zote mbili zimekwishataarifiwa kuwa mwamuzi wa mchezo huo atafahamika siku ya mchezo wakati wa kikao cha maandalizi ya mechi. (Pre-match meeting)
Alfred Lucas
Huo ni utaratibu wetu tulioamua kujiwekea bila kuangalia wengine katika mataifa mengine wanafanyaje katika derby kama hizi, tunakumbuka katika mchezo uliopita ambao ulipelekea uwanja kufungiwa, kwahiyo lazima tuchukue tahadhari. Amesema Lucas
Kwa upande wa vilabu vyote Simba na Yanga, zimeonekana kukubaliana na uamuzi huo, ambapo kwa niaba ya Yanga, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salum Mkemi amesema wao wako tayari kwa mwamuzi yeyote hata awe anatoka Simba, ilimradi afuate sheria zote za soka.