Jumatatu , 25th Mar , 2024

Klabu ya Yanga SC imetangaza kuzindua hamasa kwa mashabiki wake kesho Machi 26-2024 Jijini Dar es Salaam kuelekaea mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns wa robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika utakaochezwa Jumamosi Machi 30-2024 kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kuelekea uzinduzi huo,Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe amesema kama ilivyokuwa utaratibu wao wa kuwapa michezo ya kimataifa wachezaji na sasa mchezo huo utabebwa na Kiungo Mudathir Yahya Abbas huku kauli mbiu ni Simu ziite Tukutane Kwa Mkapa

'' Kazi ambayo tunayo kuanzia sasa hivi ni kupiga simu kwa watu wote tuwaambie tukutane kwa Mkapa” amesema Kamwe

Katika hatua nyingine,Kamwe amezungumzia maendeleo ya wachezaji waliokuwa na majeruhi kuelekea mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns huku akiishukuru TFF kwa kuwaruhusu wachezaji wao kujiunga na kambi yao iliyopo Avic Kigamboni Dar es Salaam.

“Zawadi Mauya yupo tayari kufanya kazi kubwa dhidi ya Mamelodi Sundowns, Kibwana Shomari anaendelea vizuri, Yao bado ni 50/50 alichanika nyama za paja, Pacome alikuwepo kwenye kikosi cha Ivory Coast dhidi ya Benin na yupo fit kwa zaidi ya 80% na Aucho anaendelea kujifua kujipanga dhidi ya Mamelodi Sundowns”amesema Kamwe.